Thursday, March 13, 2008
MATEPELI DAR WAMEZIDI WATUMIA USHIRIKINA
Hapa jijini kuna watu waovu sana matapeli wa kutisha na wanaojifanya kumjua Mungu sana. huwa wanajifanya wauza madini na kudanganya watu kuwa wao wanafanya kazi kwa Mzungu mmoja ambaye ana ofisi TRA Mwenge na wanamtapeli mtu kuwa atoe pesa na wakishampelekea huyo mzungu madini hayo watapata faida kubwa sana. Wakishapokea pesa huwa wanafika pale Mwenge TRA na kumwambia aliyetapeliwa subiri kidogo nikaongee naye au akiwa kwenye gari na hao matapeli wenzake anajifanya ni wageni anaenda kuwapa soda na wanaondoka pamoja kugawana pesa na kumwachia mtapeliwa madini yale ili kuhakikisha kuwa wanarudi kumbe wamefungia udongo ndani na wanapotea. Hawa matapeli wanatumia viini macho na ushirikina kudanganya watu kumbe ni wezi kupindukia. Ukiwaona wamevaa vizuri, wamefunga tai na wana magari. Ni ukweli mtupu na wametapeli watu wengi sana. Wanapofika hapo TRA Mwenge wanasimama pembeni kama mtu anayemteremsha mtu aliyempa lift na kumshusha mtapeliwa ili awasubiri.
Subscribe to:
Posts (Atom)